Hakuna mtu
aliyeumbwa ili afanye makosa,kila mtu ameumbwa ili aishi katika viwango vya juu
vya maisha na kutimiza kusudi la maisha,mtu anapoishi katika viwango vya juu na
kutimiza kusudi la maisha,huyafurahia maisha na kuona maisha ni ya thamani.
Ni hulka ya
mwanadamu kujaribu vitu vingi katika maisha yake, haswa vijana hupenda kudadisi
na kujaribu mambo mengi katika maisha, Albert Einstein alipata kusema “Kama
haujawai kufanya kosa lolote,basi haujawai kujaribu kitu chochote”,kwa mantiki
hiyo mtu anayejaribu vitu vingi,hufanya makosa mengi.
Katika kutimiza ndoto ya maisha yako,utajaribu
vitu vingi,na katika majaribio hayo kuna makosa utakayo yafanya,na haina maana
kwamba uishie hapo hapo pindi unapofanya makosa ,bali unapaswa kujifunza kutoka
katika makosa hayo,unapojifunza kutoka katika makosa,una jenga hali na ufahamu
wa kutokurudia makosa yale yale,watu wengi wanarudia makosa mara
nyingi,kwasababu tu hawana utaratibu wa kujifunza katika makosa yao,leo hii
thubutu kujifunza katika makosa yako,na si kujiona mtu usiyefaa.
Achilia mbali
makosa yanayofanywa na mtu anapotaka kutimiza ndoto zake,kuna makosa ambayo mtu
hufanya katika maisha yake ya kila siku,aidha kwa kukusudia au kwa
kutokusudia,baada ya mtu kufanya makosa mara nyingi mtu hujisikia ana hatia(guilty),wapo watu wanaotubu na wengine
wala hata hawatubu,wapo naojisamehe nafsi zao na wapo ambao hawajisamehi nafsi
zao.
Mtu anapokuwa na hatia hupoteza hamu ya
kufanya mambo makubwa (Extra ordinary
things), leo hii tuna watu wengi sana wanaoteswa na hisia za mambo
waliyofanya katika maisha yao,hawawezi kuelezea na wala hawajui wa anzaje
kueleza,wana ndoto,lakini kuta za gereza la fikra zimewazui wasitimize ndoto
zao,tuna waona wanafuraha na Amani lakini kiukweli hawana,wamefungwa kisawa
sawa.
Mimi sijui upo
gereza gani, ni wewe tu ndiye unayejua, na tena unajua umekaa gerezani kwa siku
ngapi, wiki nagapi, miezi mingapi, miaka mingapi? Hauwezi ukawa huru kama hisia
za makosa zimekufunguka, ni lazima utoke huko, kwani tangu umekuwa kwenye hilo
gereza umefaidika na nini? hakuna ulichopata Zaidi ya hisia za maumivu.
Ndoto uliyo nayo
ni kubwa sana,muda wakuanza kuitekeleza ni sasa,ili uweze kuitekeleza ni lazima
utoke gerezani,utakapotimiza ndoto yako utayabadilisha maisha yako na maisha ya
watu wengine. Wakati wako ni sasa, toka huko kwenye maumivu ya hisia za
makosa,na uishi maisha yenye furaha siku
zote.
Kwa msaada na ushauri
Na Baraka Daniel
+255762362413
0 comments:
Post a Comment